Njia nne (4) unaweza tumia kupunguza maumivu wakati wa hedhi.
1. Tumia Joto
Tengeneza joto kwa kusungua tumbo lako la chini. Fanya hivi kwa dakika chache. Au weka maji yaliyochemshwa hapo awali kwenye chupa ya maji, na uweke moja kwa moja kwenye tumbo lako la chini au uifunge kwa kitambaa.
2. Mazoezi ya Kawaida
Kama ya Kuchuchumaa Dakika 10 - 15 za Mazoezi haya Nyumbani sio mbaya. Sio lazima kwenda Gym
3. Vyakula
Punguza Vyakula vya Sukari. Epuka Vinywaji Vinavyotoa Sauti Hii ya 'kpissh!' ukizifungua. Kula zaidi Nyama, Mayai na Samaki. Na tusisahau maji.
4. Tumia Dawa
Inashauriwa, kwa maumivu ya kawaida acha tu mwili ujitibu wenyewe. Endapo maumivu ni makali basi tumia dawa za maumivu kama: Panadol, Proxican, Ibrufen au diclofenac.