Je, unakabiliwa na upungufu wa maziwa ya kunyonyesha?
Usijali, hauko peke yako. Hapa kuna vidokezo vya kukusaidia kuongeza uzalishaji wako wa maziwa:
1. Nyonyesha Mara kwa Mara
Hakikisha anashika vizuri na anyonye kila baada ya saa 2-3 wakati wa mchana.
2. Pampu baada ya kunyonyesha
Baada ya kunyonyesha, jaribu kutumia pampu kwa dakika ziada 10-15 ili kuchochea mwili wako kutoa maziwa zaidi.
3. Kunywa maji ya kutosha na kula vizuri
Kunywa maji mengi na unganisha chakula kilicho na lishe kamili kama matunda, mboga mboga, nafaka kamili, na protini nyepesi.
4. Mbegu za Maboga
Njia nzuri ya mwanamke kuongeza maziwa ya kunyonyesha ni kula vyakula vyenye uwingi wa protein kama vile Mbegu za Maboga.
5. Shauriana na mtaalamu wa afya
Tafuta ushauri kutoka kwa mshauri wa kunyonyesha au daktari wa watoto ambaye atakupa mwongozo unaofaa.