Close

Close

Anaemia(Upungufu Wa Damu) Kwa Mjamzito

Mama mjamzito anakuwa na hatari kubwa ya kupoteza uhai wake pindi ajifunguapo,sababu zoezi zima la kujifungu linahitaji damu ya kutosha ,akipoteza damu nyingi ni hatari kwake kuishiwa damu mwilini.

Dalili Za Upungufu Wa Damu Mwilini

  1. Kusikia kizungu zungu
  2. Kukosa nguvu
  3. Kubadilika rangi ya mwili kuwa mweupe kuliko kawaida , utaona viganjani, kwenye kucha, macho na ulimi
  4. Kukosa umakini wa kuona vizuri
  5. Mapigo ya moyo kwenda mbio
  6. Kushindwa kupumua vizuri
  7. Kuvimba miguu

Ushauri Juu Ya Upungufu Wa Damu Kwa Mama Mjamzito

Upungufu wa damu unaweza tibika kwa haraka na kuokoa maisha ya mama na mtoto, kinachotakiwa mama anahitaji kupima kiasi cha damu kila ahudhuriapo klinik.

Na anaweza kuongeza damu kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma kwa miligram 2-4.8 kwa siku.Kutumia vidonge (supplements) za folic acid zinasaidia kuongeza kiasi cha damu kwa haraka.

Badala ya dawa unaweza tumia chakula na matunda kama njia moja ya kutatua tatizo hili.

1. Mfano ni kutumia matunda ya beetroot unaweza yachemsha ukatengeneza juice, unanweza ukasaga ukanywa au ukapikia kwenye chakula.

2. Kutumia juice ya nyanya au rosella.

3. Kula mboga za majani spinach, mchicha, brocoli au matembele kwa wingi

4. Kula dagaa au kunywa supu ya maharagwe kwa wingi

5. Kunywa maziwa, cheese na kula mayai