Close

Close

Bawasili kwa Mjamzito

Bawasili ni nyama zinazotokea eneo la mkundu(haja kubwa) kutokana na kuvimba kwa mishipa midogo ya damu. 

Nyama hizi zaweza kuwa ndogo sana kama punje ya haragwe au zikawa kubwa zaidi kama tonge ugali na mtu mzima. 

Je bawasili kwa Mjamzito ni Tofauti?

Bawasili kwa mjamzito haina tofauti na ile ya kawaida.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anapenda kuongelea kuhusu bawasili na ndio maana unaitwa ugonjwa wa aibu. Bawasili ni kuvimba tu kwa mishipa midogo ya damu kwenye eneo lako la mkundu. Baada ya kuzaa mishipa hii inaweza kuachia na bawasili ikaisha kabisa.

Japo kila mtu anaweza kuugua bawasili lakini inawapata zaidi wenye mimba hasa katika miezi mitatu ya mwisho(third trimester) yani week 28.

Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye eneo la nyonga na mgandamizo unaletwa na kiumbe cha tumboni husababisha mishipa midogo ya damu kwenye mkundu kuanza kuvimba.

Bawasili pia inaweza kusababishwa na mjamzito kukosa choo ama kupata cho kigumu sana. Choo kinapokuwa kigumu kinakufanya utumie nguvu kubwa kujikamua ili kukitoa. Wajawazito wanapata sana shida ya choo kutokana na kupanda kwa homoni ya progesterone wakati huu wa mimba.

Dalili za bawasili

Dalili za bawasili hutegemea na aina ya bawasili inayokusumbua.Utajisikia hali hizi:

  1. Kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa
  2. Maumivu makali wakati wa kutoa haja kubwa
  3. Uvimbe kwenye eneo la haja kubwa, utagundua pale unaponawa baada ya kujisaidia
  4. Muwasho mkunduni
  5. Kujisikia kuungua katika eneo la mkundu

Je bawasili inaisha yenyewe baada ya kujifungua?

kwa wanawake wengi bawasili huisha yenyenyewe baada ya kujifungua bila kutumia dawa.

Hatua zifuatazo zitakusaidia kupunguza hatari ya kuugua bawasili wakati wa ujauzito.

Pendelea kula vyakula vyenye kambakamba kwa wingi kama maparachichi, matunda , maharage na mboga za majani katika kila mlo

Usijizuie kwenda chooni pale unapobanwa na haja kubwa

Usitumie vyoo vya kukaa vinakufaya ujikamue sana kutoa haja

Kunywa maji ya kutosha kila mara

Usitumie muda mwingi kukaa ama kusimama

Fanya mazoezi mepesi haya ya kutembea muda wa asubuhi na jioni

Wakati wa kusoma au kupumzika lala kwa upande kwa kuweka mto chini ya tumbo na kichwani