Close

Close

Hatari Ya PID Kwa Mwanamke

PID huweza sababisha matatizo yafuatayo:

  1. Ugumba (Infertility)
  2. Kansa ya shingo ya kizazi
  3. Mirija ya uzazi kuziba
  4. Majeraha kwenye mirija ya uzazi

Lakini kabla ya kuendelea tueleweshane kwanza PID ni nini?

PID au Pelvic Inflammatory Disease ni mambukizi katika via vya uzazi wa mwanamke ambavyo husababishwa na bacteria. Na huchochewa zaidi na NGONO ZEMBE.

Dalili za PID ( Pelvic inflammatory Disease ) kwa Mwanamke ni kama zifuatazo:

  1. Kutokwa na uchafu sehemu za siri yawezekana ukawa ni mweupe, njano, au rangi ya maziwa
  2. Kuwashwa sehemu za siri , pia uke kuwa laini saana
  3. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu, pia wakati wa kukojoa
  4. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  5. Homa, uchovu, kizunguzungu, kokosa hamu ya kula
  6. Mwanamke kupitia changamoto ya kupata hedhi mala mbili ndani ya mwezi mmoja

Ugonjwa wa PID kwa Mwanamke anapokaa nao kwa muda mrefu bila hata kutibiwa humfanya Mwanamke kupata tatizo la Ugumba.

Hivyo usisite kwenda hospitalini uwonapo dalili moja wapo kati ya hizo. Hili nitatizo ambalo hutibika kwa antibiotics au utumie sindano Cefriaxone ( powercelf ) inafanya vizuri saana kwenye PID