Kwa muda mreefu mwanamke amesubiria siku ya kujifungua na mtoto mpya kutokea duniani. Wanawake wanahitaji kuitambua siku hii vyema ili yasijetokea mengine mabaya.
Kwa kuwa dalili hizi zinakuja kwa namna tofauti anaweza kujikuta mjamzito akamzalia mwanae kwenye tundu la choo. Sababu ya kutokufahamu viashiria vya uchungu.
Dalili 10 Za Kukaribia Kujifungua
- Mtoto anaanza kushuka maeneo ya kwenye nyonga. Kwa wanawake wengi wanaanza kuona hali hii wiki mbili ama nne kabla ya kujifungua.
- Njia ya mimba (cervix) huanza kuachia. Hii ni sehemu inayounganisha uke na sehemu ya ndani ya mfuko wa mimba.
- Maumivu ya tumbo yanaongezeka pamoja na ya mgongo.
- Viungio vyako utaviona kama vinaachiana.
- Unaanza kuharisha.
- Kuongezeka kwa uzito kutakata kabisa uzito utakuwa hauongezeki.
- Uchovu unakuwa mkali zaidi.
- Uke unaanza kutoa uteleziutelezi.
- Maumivu ya tumbo ya mara kwa mara kuongezeka.
- Kutokwa na maji kwenye uke ambayo yanaweza yakawa na chembe chembe za damu.