1. Tazama unachokula:
Vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni. Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips.
2. Kula Mara nyingi kidogo kidogo
Badala ya kula milo mikubwa mitatu katika siku moja. Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka, usijipinde, itasaidia chakula kuteremka vizuri tumboni.
3. Masaa matatu kuelekea kulala usile chakula
Unapolala yatakiwa kuwe hakuna chakula tumboni itakusaidia kukontroo kiungulia.
4. Unapolala hakikisha unaweka mto
Hakikisha unapoenda kulala eneo la juu la kichwa linakuwa juu kidogo.
5. Vaa nguo pana zisizobana
6. Kunywa maji baada ya kumaliza kula na siyo katikati ya mlo
7. Usivute Sigara
Kemikali zilizopo kwenye sigara zinafanya kulegea kwa valve zinazouzia chakula kutoka.
8. Usitumie pombe
Pombe ni mbaya hata kwa ukuaji wa mtoto maana hupelekea mtoto kuwa na ulemavu wa ubongo na viungo. Pombe pia hufanya valve za kwenye koo la chakula kulegea na hivo kuruhusu chakula kurudi juu.