1. Njia ya kwanza ni kuepuka matumizi ya pombe, dawa za kulevya na kuvuta sigara.
Hizi ndizo njia ambazo Usababisha mimba kutoka kwa sababu baadhi ya vilevi ni vikali na kuwepo kwa nicotine usababisha kuharibika kwa mimba.
2. Fanya mazoezi mepesi mepesi.
Kwa kufanya mazoezi hayo usababisha ukuaji mzuri wa kichanga ila mazoezi makubwa makubwa achana nayo hasa kufanyanya kazi nzito ambazo Usababisha mimba kutoka unapaswa kuepukana nayo ili kuweza kuepuka na matatizo ya kutoka mimba.
3. Jikinge na Maambukizi mbalimbali hasa kwenye via vya uzazi.
Wakati wa ujauzito ni vizuri kabisa kujikinga na kuwepo kwa magonjwa kwenye via vya uzazi kwa sababu yanaweza kusababisha maambukizi.na kusababisha mimba kutoka kwa hiyo na siku zote epuka kujamiiana na wanaume wengi au mbalimbali wakati wa ujauzito ili kupunguza magonjwa.
4. Na pia wakati wa ujauzito ni vizuri kuepuka kutumia sabuni za kunukia.
Kusafisha uke daima tumia sabuni ya kawaida kwa sababu kuna hatari ya kuua bakteria wazuri wa kulinda uke na kusababisha Maambukizi kwenye via vya uzazi na kusababisha mimba kutoka.
5. Punguza matumizi ya vyakula visivyofaa.
Kwa kawaida kuna vyakula ambavyo havifai wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha caffeine kwa mfano kahawa na matumizi ya mara kwa mara ya soda .
6. Tumia mlo kamili wakati wa ujauzito.
Kwa kawaida mlo kamili unatakiwa wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula na mboga mboga za majani na pia matumizi ya vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kwa kufanya hivyo tunaweza kupunguza kiwango cha mimba kuharibika