Close

Close

Tendo la Ndoa Baada ya Kujifungua

Baada ya kujifungua, mwanamke anatakiwa kusubiri siku 42, yaani wiki 6 ndipo aanze tena kushiriki tendo la ndoa. Muda huu unahusisha aina zote za kujifungua.

Kitu cha muhimu kuzingatia ni kuhakikisha kuwa damu na majimaji ya uzazi vimeacha kutoka pamoja na saikolojia ya mwanamke kukaa vizuri katika kushiriki tena tendo hili.

Kwa wanawake waliojifungua kwa njia ya upasuaji, wanapaswa kushiriki tendo la ndoa kwa mitindo isiyoumiza mishono yao. Itasaidia uponaji wa haraka na kuepuka maumivu wakati wa tendo.