Hapa tutakuelewesha Ugumba ni nini, aina za ugumba, sababu za ugumba kwa mwanamme na mwanamke, na tiba ya ugumba kwa mwanamke.
Ugumba ni kile kitendo au ni ile hali ya mwanamme na mwanamke kujamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kinga yoyote na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito. Linapotokea tatizo hili, wote wawili wanatakiwa wapimwe ili kujua ni nani kati yao ndiye chanzo cha tatizo.
AINA ZA UGUMBA
Ugumba upo wa aina mbili primary na secondary.
Primary ni kushidwa kupata mtoto kwa kipinda cha mwaka mmoja japo wawili hao wanakutana ki mwili bila kutumia kinga yeyeto na bila kuzingatia calendar au mzunguko wa hedhi.
Na Secondary ni pale ambapo mama anapata mtoto mmoja tu nakushidwa kupata mwengine.
SABABU ZA UGUMBA
Sababu zinaweza kugawanyika kwa wote wawili inaweza ikawa Baba ndio anashida au Mama ndio mwenyeshida.
Tuanze na sababu za mwanaume kushidwa kumpatia mke ujauzito:
- Msongo wa mawazo
- Ukosefu wa homoni za kiume za kutosha
- Uvutaji wa sigara
- Unywaji wa pombe
- Asili & Ulaji mmbovu
Na Kwa Mwanamke Sababu Zinaweza Kuwa Zifuatazo:
1. Utoaji Wa Mimba;
Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza kusababisha ugumba usiotibika.
2. Matatizo Ya Vizaalishaji Vya Mayai (Ovari);
Ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini kuna magonjwa ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst.
3. Matatizo Ya Mirija Ya Uzazi;
Ovari zimeunganishwa kwenye mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi..wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.
4. Matatizo Ya Kizazi;
Kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba. mfano, makovu ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kadhalika.
5. Kansa;
Kansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujiweka kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa kabisa.
6. Matatizo Ya Mlango Wa Uzazi;
Oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.
7. Magonjwa Mengine Ya Mwili;
Magonjwa yeyote ya binadamu ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika.
8. Matumizi Ya Sigara Na Pombe;
Unywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.
9. Msongo Mkubwa Wa Mawazo;
Ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha inasababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama gonadotrophin releasing hormone hivyo hali huzidi kua mbaya.
10. Uzito uliopitiliza;
Mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni moja ya anjia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia ugumba.
DALILI ZA UGUMBA
Dalili hizi zinaweza ashiria mwanamke anaweza kuwa na tatizo la ugumba.
- Hedhi kupishana
- Hedhi kutoka kidogo sana
- Hedhi kutoka nyingi sana
- Maumivu makali ya tumbo wakati kabla au baada ya hedhi
- Kutopata hedhi au hedhi kuruka miezi au kurudia ndani ya mwezi mara mbili
- Kuhisi mara kwa mara hali ya ujauzito na kila ukipima ni negative
- Kutopata hamu ya tendo la ndoa
TIBA YA UGUMBA
Baada ya maelezo ya mwathirika kuhusu tatizo lake la kutopata ujazito, dakatari anaweza kuamua kuchukua vipimo ili kujua aina ya tatizo linalomsumbua mama huyo na ndipo tiba itakapotolewa kulingana na aina ya tatizo litakaloonekana.
Katika ukurasa huu tutaona baadhi ya njia zinazotumika kumsaidia mwanamke mwenye tatizo la kutopata mimba.
Aina Za Tiba Ya Ugumba Kwa Wanawake
Tiba itakayotolewa kuondoa tatizo la mwanamke kutopata ujauzito itategemea aina ya tatizo lililobainika, umri wa mwanamke na tatizo hilo limedumu kwa muda gani.
Kwa vile ugumba ni tatizo gumu kulitibu, tiba inaweza kutumia kiasi kikubwa cha pesa, muda mrefu na kuhitaji uvumilivu kisaikolojia.Pamoja na kuwa kuna wanawake wanaofanikiwa kupata ujauzito baada ya kupata aina moja au mbili tu za tiba, si jambo la ajabu kama mwanamke mwingine akahitaji kupata mchanganyiko wa aina nyingi zaidi wa tiba kabla hajafanikiwa kupata mimba.
Tiba za ugumba hujaribu kurudisha uwezo wa mwanamke kupata ujauzito – kwa kutumia dawa au upasuaji – au kumsaidia mwanamke kupata mtoto kwa njia nyingine za kitaalamu.
Hizi njia ni kama zifuatazo:
A) NJIA YA DAWA
Madawa hutumika ili kuboresha au kurudisha uwezo uliopotea wa kuzalisha mayai – hii ndiyo njia kuu inayotumika kumsaidia mwanamke mwenye tatizo la kuzalisha mayai. Dawa hizi hufanya kazi kama homoni za kawaida za mwili za follicle-stimulating.
Dawa Ya Ugumba Kwa Wanawake
1. Follicle-Stimulating Hormone (FSH) na Luteinizing hormone (LH):
Kuamsha uzalishaji wa mayai. Dawa hizi pia hutumika kuwasaidia wanawake wenye uwezo wa kuzalisha mayai kutoa mayai yenye ubora zaidi au kutoa yai zaidi ya moja.
2. Clomiphene citrate:
Clomiphene citrate (Clomid, Serophene) ni dawa ya kunywa inayosaidia tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating hormone FSH na luteinizing hormone LH kwa kiwango kikubwa zaidi hivyo kusaidia ukuaji wa ovarian follicle inayotunza yai.
3. Gonadotropins:
Hizi ni dawa za sindano zinasaidia ovari moja kwa moja kwa kusaidia ukuaji wa yai na utoaji wa yai kwa wakati unaotakiwa.
4. Metformin:
Hizi hutumika wakati inapobainika kuwa mwili kushindwa kuitumia insulin ndicho chanzo cha ugumba.
5. Letrozole:
Hii hufanya kazi kama clomiphene kusaidia mwili kutoa yai.
6. Bromocriptine:
Hii hutumika wakati matatizo ya ugumba yanatokana na tezi za pituitary kutengeneza prolactin (hyperprolactinemia) nyingi kupita kiasi.
B) NJIA YA UPASUAJI
Kuna baadhi ya operesheni ambazo hufanywa kurekebisha dosari zilizoonekana au kuboresha uwezo wa mwanamke kuzaa. Hata hivyo, operesheni hizi zimepungua umaarufu wake baada ya njia bora na za kisasa kugundulika.
1. LAPAROSCOPIC OR HYSTEROSCOPIC SURGERY
Upasuaji wa aina hizi mbili huweza kuondoa au kurekebisha dosari katika tumbo la uzazi la mwanamke. Urekebishaji wa umbo la nyumba ya uzazi, kuondoa endometriosis na baadhi ya aina za uvimbe (fibroids) na kuongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba.
2. TUBAL SURGERIES
Pale inapogundulika kuwa mirija ya uzazi imeziba au imejaa maji (hydrosalpinx), laparoscopy mara chache huweza kutumika kuongeza kipenyo cha mirija au kutoboa njia nyingine katika mirija hiyo.
Kuongeza uwezekano wa kupata mimba kwa kutumia in vitro fertilization (IVF), kuiondoa mirija ya uzazi au kuiziba karibu na nyumba ya uzazi ndiyo njia inayopendekezwa pale mirija ya uzazi inapokuwa imejaa maji.
3. Intrauterine Insemination (IUI)
Hii ni njia ya kumsaidia mwanamke kupata ujauzito inayotumika kama mwanamme ni mgumba, mwanamke ana matatizo ya ute (cervical mucus) au kama ugumba haujaeleweka chanzo chake.
Njia hii ambayo pia huitwa artificial insemination, hufanywa kwa kupandikiza mamilioni ya mbegu komavu ndani ya tumbo la uzazi (uterus) la mwanamke anapokaribia siku zake za kutoa yai.
4. Assisted Reproductive Technology
Njia hizi ni ghali sana na hutumia muda mrefu lakini zimewasaidia watu wengi ambao vinginevyo hawangeweza kupata watoto katika maisha yao. Hizi njia ni kama:
i. In vitro fertilization (IVF):
Katika moja ya njia hizi, mayai yaliyokomaa huchukuliwa kutoka kwa mwanamke kisha kuchanganywa na mbegu za mwanamme kwenye maabara. Embryo zinazotokea hurudishwa kwenye nyumba ya uzazi ya mwanamke ili ziweze kukua.
Hii huitwa In vitro fertilization (IVF). Ni njia bora kwa mwanamke ambaye mirija yake ya uzazi imeziba au kama mwili wa mwanamme hauna uwezo wakuzalisha mbegu za kutosha.
ii. Zygote Intrafallopian Transfer (ZIFT) Au Tubal Embryo Transfer:
Njia hii inafanana na ile ya in vitro fertilization ambapo mayai na mbegu huchanganywa kwenye maabara. Hapa embryo hupandikizwa kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes) badala ya kuwekwa kwenye nyumba ya uzazi (uterus).
iii. Gamete intrafallopian transfer (GIFT):
Mayai na mbegu za mwanamme huwekwa kwenye mirija ya uzazi na kuruhusu embryo kuundwa ndani ya mwili wa mwanamke.
iv.Intracytoplasmic sperm injection (ICSI):
Ni njia inayotumika pale inapobainika kuwa mwanamme ana matatizo ya kuzalisha mbegu bora. Hapa mbegu moja hudungwa kwenye yai la mwanamke lililokomaa na embryo kupandikizwa kwenye nyumba ya uzazi (uterus) au kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes).